1.0.HISTORIA FUPI YA WILAYA:
Wilaya ya Kilolo ilianzishwa mwaka 2005 kwa tangazo la serikali Na.220 baada ya kugawanywa toka wilaya ya Iringa. Hivyo kwa kipindi cha mwaka 1961-2005 Wilaya ya Kilolo ilikuwa ni sehemu ya Kata na Tarafa za Wilaya ya Iringa.
1.1.Mahali Wilaya ilipo
Wilaya ya Kilolo ipo kati ya nyuzi za Latitude 70 – 8.30 Kusini mwa mstari wa Ikweta na nyuzi Longitude 340 – 370 Mashariki mwa mstari wa “Greenwhich”. Wilaya imepakana na Wilaya ya Mpwapwa (Dodoma) upande wa Kaskazini, Wilaya ya Kilosa kwa upande wa Kaskazini Mashariki na Wilaya ya Kilombero kwa upande wa Mashariki katika Mkoa wa Morogoro.Kwa upande wa Kusini ni Wilaya ya Mufindi wakati upande wa Magharibi imepakana na Wilaya ya Iringa (Vijijini).
1.2.Eneo la Wilaya
Wilaya ya Kilolo ina eneo lenye ukubwa wa jumla ya km2 7,882 Wastani wa asilimia 86.32 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km2 6803.2 Eneo linalobakia la km2 1077.8 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama, milima na misitu.
2.1Utawala
Wilaya ya Kilolo imegawanyika katika Tarafa tatu ambazo ni Kilolo, Mazombe na Mahenge. Aidha Wilaya ina Kata 24 na Vijiji 94, Mitaa 16 katika mamlaka ya mji mdogo Ilula na vitongoji 499
Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya
Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo
Simu ya mezani: 0262968010
Mobile:
Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz
Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa