• Kero |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Kilolo District Council
Kilolo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo,Umwagiliaji na ushirika
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi,Maliasili na Mazingira
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu
      • Ufugaji
    • Afya
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Customers services agreement
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofis au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

JUKWAA LA UWEZESHAJI KIUCHUMI KWA WANAWAKE NGAZI YA WILAYA LA ZINDULIWA

Posted on: May 18th, 2017

Jukwaa hilo lilizinduliwa rasmi tarehe 17/05/2017 na Mh.Asia Juma Abdalah mkuu wa Wilaya ya Kilolo.Lengo la kuanzisha jukwaa la Uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ni kukutana na kujadiliana fursa,changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli zingine za kiuchumi.Vilevile kuongeza uelewa wa wanawake katika uchumi,biashara,upatikanaji wa mtaji,sheria za nchi katika masuala ya uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi.

Wanawake wamekuwa hawapati fursa za kutosha za kiuchumi hapa Tanzania na duniani kote. Hii inatokana na kutokuwa na usawa katika Fursa, uwezo wa kupata mitaji, ajira na baadhi ya maeneo malipo ya kazi kwa wanawake yamekuwa sio sawa na wanaume. Kuondoa matabaka na sheria ambazo zitasaidia kuondoa ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake ni jambo la muhimu sana kuleta maendeleo ya usawa katika pato la Taifa, jamii na familia. Ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi ni kichocheo kizuri cha maendeleo ya nchi yetu na jamii kwa ujumla.

Katika kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu ambayo pia yamesisitiza uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, katibu mkuu wa umoja wa Mataifa aliteua timu ya viongozi na wataalam ambao wanafanya kazi kama chombo cha juu katika kutambua na kuweka mikakati ya kupunguza na kuondoa pengo kubwa ambalo limejengeka duniani na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi duniani kote.

Timu hii inaangalia mambo muhimu ambayo yatasaidia kurekebisha hali iliyopo sasa. Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kwa kuhakikisha Malengo ya Maendeleo endelevu yanafikiwa na malengo ya 50/50 ya dunia kufikiwa mwaka 2030.
Katika timu iliyoteuliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Mh. Makamu wa Rais mama Samia Hassan Suluhu ni mjumbe, hivyo Mh.  Makamu wa Rais ameelekeza kuwepo na Majukwaa ya Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi katika Mikoa yote na Halmashauri zote za Tanzania. Majukwaa haya yatasaidia kuongeza uelewa wa wanawake katika Uchumi, biashara, upatikanaji wa mitaji, sheria za nchi katika masuala ya Uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi.
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni chombo ambacho kilianzishwa ili kuratibu na kuongoza shughuli zote za uwezeshaji wananchi kiuchumi zinazoendeshwa na Sekta ya Umma na Binafsi. Baraza pia linasimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kuwaongoza watanzania kwenye uchumi imara na kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara na uchumi shirikishi yanakuwepo.Aidha Mh.Bi Asia Abdalah alisisitiza wajumbe wote ambao wako kwenye hilo jukwaa "ni wajibu wetu sasa sisi ambao tuko kwenye chombo hiki kuhakikisha miongozo,maelekezo na taratibu zote ambazo tunapewa na wataalamu wetu tunazifanya nukta kwa nukta neno kwa neno mstari kwa mstari na hivyo ndivyo ambayo tunaweza kubadilisha maisha".Pia mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Valence Kihwaga aliwataka waratibu wa majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi ngazi ya kata yakafanye kazi kushirikiana na wananchi ili jukwaa hili litakapo kutana kwa mara ya pili kufanya tathimini  yale yaliyopendekezwa kwenye uzinduzi wa jukwaa yawe yamefanyiwa kazi kwa lengo la kuleta mabadiliko



Matangazo

  • Malipo ya Tasaf Wilaya ya Kilolo kuanza tarehe 27/03/2017 hadi 30/03/2017 March 23, 2017
  • Easter March 24, 2017
  • Tangazo la Mauzo ya Viwanja May 08, 2017
  • Mazoezi ya Pamoja Tarehe 13 Mei May 10, 2017
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO YANG'ARA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE 2017

    August 11, 2017
  • JUKWAA LA UWEZESHAJI KIUCHUMI KWA WANAWAKE NGAZI YA WILAYA LA ZINDULIWA

    May 18, 2017
  • Mh.JAFO SULEIMAN SAID AKIKAGUA UJENZI WA MAJENGO YA HOSPITALI YA WILAYA YA KILOLO UNAVYOENDELEA

    May 16, 2017
  • MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA BILIONI 14.9 YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU 2017

    April 26, 2017
  • Angalia zote

Video

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa akitoa ujumbe wa mwenge 2017
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Tangazo la Ajira

Viungio vinavyohusiana

  • Public Service Management
  • Watumishi Portal
  • PO-RALG
  • National Examination Council
  • eGA
  • Mkoa wa Iringa
  • Mufindi DC
  • Iringa DC
  • Iringa MC

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtengaji wa Wilaya

    Postal Address: S.L.P 2324 Kilolo

    Simu ya mezani: 0262968010

    Mobile:

    Anuwani ya barua pepe: ded@kilolodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Onyo
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hati miliki @2017 Halmashuri ya Wilaya ya Kilolo.Haki zote zimeifadhiwa